Header

Picha: Mastaa wa Uganda wafurika kwenye misa ya mazishi ya Ivan

Nje ya kanisa la Namirembe mjini Kampala, Uganda, ambako kumefanyika misa ya kumuaga Ivan Semwanga, paliegeshwa magari ya kifahari ambapo mengi yakiwa na plate number za majina ya wamiliki.

Mastaa wa Uganda na viongozi wa serikali, walikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria. Ulinzi ulikuwa mkali kuhakikisha shughuli inamazilika salama. Bebe Cool na mkewe, Zuena walikuwa miongoni mwa waliohudhuria, huku kwenye picha moja aliyoiweka Zari Instagram, Zuena anaonekana akiwa amkemkumbatia Zari. Wengine waliohudhuria ni muimbaji King Saha pamoja na Radio.

Alikuwepo pia mfanyabiashara tajiri, Jack Pemba. Zari alikuwa amevaa nguo nyeusi huku nywele zake akiwa amefunga kilemba cha rangi hiyo.

Tazama picha zaidi hapo chini:

Comments

comments

You may also like ...