Header

‘Sisi wasanii tunapata hela, wasanii wanapenda starehe’ – Dully Sykes

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na hatmaker wa ngoma ya ‘Bongo fleva’ na ‘Yono’ Abdul Sykes a.k.a Dully Sykes amesimulia sababu za nini kilimsukuma kununua na kutengeneza mazingira ya kuwa na Studio ya kuandaa muziki.

Akizungumza na Dizzim Online Dully amesema kuwa kikubwa kilichomsukuma mpaka kumiliki studio kama msanii ni kuepuka usumbufu katika muziki wake pia kupata uhuru wa kufanya mambo yake kama msanii kwa muda wowote anapohitaji kufanya jambo lolote linalohusu muziki.

“Nilifikiria nikaona kwamba nafanya muziki, kama napata idea siwezi kwenda kumgongea mtu nikamwambia kwamba naomba kurecord wakati mtu kajipumzika No! kama nina studio yangu naweza kurecord mwenyewe. Sisi wasanii tunapata hela, wasanii wanapenda starehe tu. Kwahiyo Equipments ni vitu ambavyo unaweza kununua kama ukiwa na akili hata kwa hela ndogo unayoipata” Amesema Dully.

Hata hivyo Dully ameongeza kuwa baada ya kupiga hatua mpaka kumiliki bendi na vifaa vya studio vyenye viwango ameona ni vyema kuanzisha record lebo hatua ambayo ameitaja kama moja mafanikio ya muziki wake kwa kipindi chote cha kufanya muziki.

 

 

Comments

comments

You may also like ...