Header

Mavideo Queen wanaoimba wameharibu muziki wa Tanzania- Baby Madaha

Muimbaji na muigizaji wa filamu, Baby Madaha amezungumzia mabadiliko ya muziki ulikinganisha na miaka kadhaa iliyopita. Ameiambia Dizzim Online kuwa muziki wa sasa unahitaji fedha na kama huna ni ngumu kufanikiwa. Ameongeza kuwa hiyo ndio sababu kumeibuka mavideo queen wengi ambao wameingia kwenye muziki lakini hawana kipaji.

“Muziki wa sasa hivi lazima uwe na pesa ili uweze kupromote kama mavideo queen wanatoa muziki wa ajabu ajabu halafu unapigwa kwenye radio. Hiyo yote sasa hivi ni kwasababu wanashika pesa, yaani muziki tena sasa hivi sio wa talent kama ulivyokuwa zamani muziki sasa hivi hela yako hawa mavideo queen wanaharibu tu,” amesema Baby.

Aliongeza na kusema, “Na kwa mwenendo huu hatuwezi kufika mbali kwasababu mtu hajui kuimba anatoa ngoma anatoa na video anaonesha onesha maungo yake kwenye hiyo video yake haimbi kitu chochote kile cha maana. Yaani vitu anavyovifanya anachochea ngono inapelekea sasa watu kuzidi kuamini kwamba hii tasnia ni ya kihuni yaani muziki wa Tanzania umevamiwa, wenye vipaji sasa hivi hawaonekani kabisa,” amesisitiza.

Comments

comments

You may also like ...