Header

Tiger Woods aomba radhi kwa kukamatwa akiendesha gari akiwa amelewa, hatarini kupoteza wadhamini

Bingwa wa zamani wa mchezo wa golf, Tiger Woods ameomba radhi baada ya kukamatwa na polisi huko Florida akiendesha gari akiwa amelewa (DUI). Alikamatwa mida ya saa 9 usiku, Jumatatu na kushikiliwa katika gereza la Palm Beach County saa nne asubuhi.

Kwa mujibu wa TMZ, Woods alikuwa akiendesha gari aina ya Mercedes ya mwaka 2015. Polisi wamedai kuwa walimuona akiendesha gari kwa fujo na akiyumba barabarani na kumsimamisha.

Wanasema alikuwa akinuka harufu ya pombe na akaanza kuwa mkali. Walimuambia apumie kwenye kifaa cha kupimia wingi wa pombe lakini alikataa. Kwa Florida hiyo hupelekea kukamatwa na kusimamishwa kwa leseni ya kuendesha gari. Woods ametoa maelezo ya kilichotokea na ameoamba radhi huku akisema kuwa alikuwa hajanywa pombe bali ni mchanganyiko wa dawa alizokuwa anatumia.

Chini ni maelezo yake:

I understand the severity of what I did and I take full responsibility for my actions. I want the public to know that alcohol was not involved. What happened was an unexpected reaction to prescribed medications. I didn’t realize the mix of medications affected me so strongly. I would like to apologize with all my heart to my family, friends, and the fans. I expect more from myself, too. I will do everything in my power to ensure this never happens again. I fully cooperated with law enforcement, and I would like to personally thank the representatives of the Jupiter Police Dept. and the Palm Beach County Sheriff’s Office for their professionalism.

Tukio linaweza kuwa na madhara makubwa katika mikataba yake ya matangazo ambazo humuingia zaidi ya dola milioni 45 kila mwaka.

Comments

comments

You may also like ...