Header

Busu lamponza mchezaji wa Tenisi ‘French Open’

Mchezaji wa Tenesi Maxime Harmou amefungiwa kushiriki mashindano ya French Open na waandaaji wa michuano hiyo inayoendelea jijini Paris nchini Ufaransa  baada ya kulazimisha kumpiga busu mwandishi wa kike wa Television hadharani, alipokuwa akifanyiwa mahojiano mubashara siku ya Jumanne.

Mfaransa huyo aneshikilia nafasi ya 287 kwa ubora Duniani kwa upande wa wanaume alimpiga busu mwanadada kutoka kituo cha Eurosport, Maly Thomas huku akimpapasa maungo yake licha ya mwanadada huyo kuonekana akijitahidi kumzuia mchezaji huyo.

Shirikisho la mchezo wa Tenesi nchini Ufaransa (FTT) limetangaza kumfungia Harmou kwa muda wote wa mashindano hayo huku likiendelea kujadili suala hilo na huenda akapatiwa adhabu nyingine.

Baada ya kufanya tukio hilo Harmou, 21 aliomba msamaha kwa mwandishi huyo pamoja na kituo chake cha kazi cha Eurosports wakati alipohojiwa na Gazeti la I’Equipe kutoka nchini Ufaransa.

‘nipo tayari kumuomba msamaha yeye binafsi kama atakuwa tayari, najifunza kila siku kupitia makosa ili niwe mtu mzuri na mchezaji bora wa tenesi. Alisema Harmou ambae amepoteza mchezo katika mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo ya French Open.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kufanya tukio baya katika mashindano haya, siku ya ijumaa aliondoka kati kati ya mahojiano na mwandishi wa habari baada ya kuulizwa swali ambalo hakulipenda na alitoa lugha mbaya.

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...