Header

Dogo Janja aizungumzia siri ya ndoa na Mpenzi wake (+Video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, na hitmaker wa ‘My life’ aliyotayarishwa chini ya Marco Chali, Carl Hovind na Daxo Chali katika studio za MJ Records ‘Dogo Janja’ ametaja kipindi ambacho atamfichua mpenzi wake kama muda sahihi kwake kuruhusu wadau na mashabiki kumuona.

Akizungumza na Dizzim Online, Janja amesema kuwa mashabiki na wadau wamemjua kipitia muziki wake hivyo maisha ya mahusiano kwake atayaweka wazi pindi atakapo funga ndoa.

“mimi nipo kwenye mahusiano lakini watu wamenijua kipitia muziki wangu so siku nikija kumuweka mwanamke wangu official kwamba ninaoa…ndo mtamjua” Amesema Dogo Janja.

Yatazame mahojiano na Dogo Janja.

 

 

Comments

comments

You may also like ...