Header

Testimonial ya Carrick yasogezwa mbele

Kiungo wa Manchester United Michael Carrick amelazimika kusogeza mbele mechi ya heshima kwaajili yake iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi hii ili kupisha tamasha lililoandaliwa kwaajili ya kumbukumbu ya tukio la mlipuko wa bomu lililotokea jijini Manchester Mei 22 mwaka huu.

Mchezo huo umesogezwa mbele mpaka siku ya Jumapili Juni 4 utakaofanyika katika uwanja wa Old Traford ambapo kikosi cha United kilichoshinda taji la UEFA mwaka 2008 dhidi ya kikosi bora cha Michael Carrick anachokipendekeza Carrick.

Michael Carrick amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na Manchester United wiki moja iliyopita ataongoza kikosi kilichotwaa Ubingwa wa UEFA mwaka 2008 chini ya Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson dhidi ya kikosi cha wachezaji ambao ni bora kwa kiungo huyo ambacho kitakua chini ya Harry Redknapp.

 

Comments

comments

You may also like ...