Header

Tiger Woods alikutwa amelala kwenye usukani, uchunguzi wabaini hakuwa amekunywa pombe

Polisi wamebaini kuwa mchezaji wa golf wa Marekani, Tiger Woods hakuwa amekunywa pombe wakati walipomkatama kwa kosa la kuendesha gari akiwa ametumia kilevi.

Walimkuta akiwa amelala kwenye usukani kwenye barabara ya njia sita huko Florida. Gari hilo lilikuwa limewaka huku uongeaji wake ukiwa wa shida na hakuwa akijua umbali wa nyumbani kwake alikokuwa akienda.

Kwenye maelezo yake, Woods alisema alikuwa anatumia dawa za hospitali. Polisi wanasema alionesha ushirikiano japo alipata shida kufumbua macho yake. Imebainika kuwa Woods alikuwa ametumia dawa aina nne za kupunguza maumivu ambazo aliambiwa kutumia baada ya kufanyiwa upasuaji.

Comments

comments

You may also like ...