Header

Toxstar amuhusisha wakili wake juu ya ‘Ma Ole’ ya Belle 9 na G Nako

Baada ya hit song ya ‘Ma Ole’ ya Belle 9 pamoja na G Nako kuzua gunzo mara tu ilipotoka kufuatana na malalamiko ya umiliki kutoka kwa Tox Star kuwa wazo la wimbo huo limechukuliwa katika wazo la wimbo wake uliotoka mwanzoni mwa mwaka jana wa ‘Ole’

Katika hatua za kuujua ukweli katika mohojiano na vituo tofauti tofauti Belle 9 na G Nako walikanusha kuhusika kivyovyote katika matumizi ya wazo la wimbo wa Tox Star ambapo G Nako amesema kuwa sio rahisi kwake kutumia wazo la wimbo wa msanii wenzake ili kufanikisha kuandaa kazi zake huku Belle kusikika kwa kusema kuwa hamfahamu Tox Star.

Akisikika kupitia Planet Bongo na East Africa Radio ‘Tox Star’ amesisitiza kuwa wazo la wimno wa Ma Ole ni lake na yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo na wakakili wake ili kufuata hatua za kisheria ili apate haki zake za wazo la wimbo wa ‘Ma Ole’ na ‘Ole’.

“Natetea haki yangu, nipo kwenye haki yangu na Belle 9 analitambu hilo, timu yake nzima wanalitambua hilo kwa hiyo nitafika nao mpaka ambapo mimi nitaona kwamba niamue nimaliane nao vipi, nitajua niamlizane nao vipi. Wakili wangu nilikuwa namsubiri leo anaingia nitakaa naye chini tutadiscuss tujue tunafanyaje…I think haya mambo yatafika mbali zaidi” Amesema Tox Star.

 

Comments

comments

You may also like ...