Header

Davido sasa baada ya ‘IF’ ni ‘FALL’

Msanii mnigeria mwenye asili ya Marekani David Adedeji Adeleke ‘Davido’ baada ya kuingia katika orodha ya wasanii walioachia ngoma na zilizofanya vizuri na ngoma yake ya ‘If’ awataka mashabiki wajiweke tayari tena kwa jiwe lingine mwanzoni mwa mwezi huu.

Katika kungoja ujio wake mwingine Davido ambaye kwasasa anasemwa zaidi kupitia bifu yake na mkali mwenzake kutoka Nigeria ‘Wizkid’ ameweka mfululizo wa tatu hivi katika ukurasa wake wa Instagram zilizoambatana na maelezo mafupi ya ‘FALL 02/06/17’ yanayowaacha mashabiki katika mawazo na hamu ya kungoja kitakacho dondoshwa mara hii.

Kupia moja ya picha alizopost Davido ilibainika wazi kuwa ni ujio wa ngoma ambayo tayari itamabatana na video kabisa hata katika picha hiyo kuonekana kuwa muogozaji wa video ya wimbo huo uliotajwa kwenda kwa jina la ‘FALL’ kuwa ni DAPS.

 

FALL 02/06/17

A post shared by Davido Adeleke (@davidoofficial) on

Hata hivyo bila shaka inakumbukwa kuwa Davido ni mwenye kumbukumbu kuhusu kuokoa uhai wa shabiki yake wa kike alisema kuwa namkubali sana ‘Davido’ na kazi zake alisambaza video mitandaoni akisikika kuahidi kujiua kama hatafanikiwa kuonana na Davido kufikia siku ya kuzaliwa kwake mwezi wa nane taarifa ambayo ilimfikia Davido hata kuahidi kushiriki katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa shabiki huyo kama njia ya kuokoa maisha yake.

Comments

comments

You may also like ...