Header

Maua Sama aonywa juu ya Madawa ya kulevya

Msanii wa muziki kizazi kipya,staa wa muziki wa reggae na hitmaker wa ngoma ya ‘Main Chick’ kutoka Tanzania ‘Maua Sama’ amefichua kikubwa ambacho wazazi wake umhasa zaidi katika maisha yake na kufanya muziki.

Akizungumza na Dizzim Online Maua amesema kuwa kikubwa ambacho wazazi umhasa zaidi ni kutojihusisha na madawa ya kulevya kutoka na kile kinachoonekana kwa baadhi ya mastaa kujikuta katika ushawishi na maisha ya matumizi ya madawa ya kulevya maina ya maisha ambayo matokeo yake ni mabaya zaidi.

“mama hasa hataki nivute madawa ya kulevya, hataki kabisa…kila siku tena sio yeye tu hata baba yangu waga wakiongea na mimi waga wanajitahidi kuni-emphasize nisivute madawa ya kulevya” Amesema Maua Sama.

Hata hivyo Maua amewashuru zaidi wazazi wake hata kuwataja kuwa wamechangia pakubwa sana katika hatua zake na maendeleo katika muziki wake.

Comments

comments

You may also like ...