Header

Otile Brown autumia muziki wake kuwasahaulisha matatizo mashabiki wake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya ‘Otile Brown’ ameto sababu zake ya msingi kuimba zaidi mawazo kuhusu mapenzi katika nyimbo nyingi anaoandaa kwa ajili ya mashabiki wa muziki wake na wapya.

Akipiga stori na Mpasho nchini Kenya, Otile amejibu kuhusu mfumo wake huo wa kufanya ngoma za mapenzi na kueleza kuwa kwa upande wake kufanya kazi kama msanii ni kutengeneza mazingira ya furaha na burudani na sio kuwakumbusha matatizo mashabiki zake.

“lazima tuangalie kitu gani kinauza…unajua life is too hard enough sio vizuri kuanza kuwakumbusha watu amatatizo yao…mapenzi yana-run dunia na muziki wangu wanaweza kurelate more than kuwakumbusha watu matatizo” Amesema Otile Brown.

Hata hivyo Otile Brown ameongeza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Kistaarabu’ ulikuwa na wazo tofauti ambalo alimshirikisha Sanaipei kabla ya kuubailisha.

Comments

comments

You may also like ...