Header

‘Simba haponi taratibu kama Binadamu’: Zlatan Ibrahimovic

Hayo ni maneno aliyoandika mchezaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic katika ukurasa wake wa Instagram yaliyosomeka “Lions don’t recover like Humans” yaani Simba haponi kama Binadamu akimaanisha ameanza kurejea katika hali yake mapema  baada ya kuanza kufanya mazoezi ikiwa ni mwendelezo wa safari yake ya  kurejea tena uwanjani tangu alipopata majeruhi.

Ibrahimovic aliumia katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Europa dhidi ya Anderlecht Aprili 20 katika uwanja wa Old Traford. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 amekosa mechi muhimu katika klabu yake ikiwemo Fainali ya kombe hilo la Ulaya dhidi ya Ajax iliyofanyika nchini kwao Sweeden.

Mchezaji huyo alitazamiwa kuwa nje kwa miezi tisa, taarifa iliyotolewa na madaktari nchini Marekani baada ya kufanyiwa vipimo lakini huenda nyota huyo akarejea mapema uwanjani kutokana na kuanza kufanya mazoezi mepesi mapema.

Zlatan Ibrahimovic ni mchezaji huru, amemaliza mkataba wake na Manchester United msimu huu ingawa kuna taarifa kuwa mchezaji huyo angependa kuendelea kucheza klabuni hapo licha ya vilabu vingi kumtaka.

Comments

comments

You may also like ...