Header

Amini hiki kilifanyika kati ya Lava lava na Shilole

Msanii wa muziki wa kizazi kutoka Lebo ya WCB mwenye utambulisho wa ngoma mpya inayokwenda kwa jina ‘Bora Tuachane’ ‘Abdul Juma Mangala’ a.k.a Lava lava amefichua kushiriki kumuandikia wimbo hitmaker wa ngoma ‘Hatutoi kiki’ ‘Zuwena Mohamed’ maarufu kama Shilole.

Akizungumza na Mambo Mseto ya Radio Citizen Lava lava amesema kuwa mbali na kumkubali sana Shilole amekuwa mmoja kati ya wasanii ambao wamemthamini na kumshauri zaidi kwa kipindi chote kabla ya kusikika bila kijali udogo aliokuwa nao hata kumshirikisha katika uandishi wa nyimbo ambapo  alimuandikia wimbo wa ‘Nyang’a nyang’a’ wimbo ambao aliukubali, kuurecord kisha kuuachia.

“kuna huu wimbo wa Shilole unaitwa Nyang’a nyang’a mimi ndo niliandikaga, yah! miaka ya nyuma sana. Shilole tangu niko huko mtaani alikuwa anaweza akanipigia simu akaniambia dah! mdogo wangu safari ni ndefu komaa utafika, kuna siku utafika…ulikuwa hajali kama mimi ni underground wala nini” Alisema Lava Lava.

Hata hivyo katika mahojiano hayo Meneja wa msanii Diamond Platnumz ‘Babu Tale’ aliongeza kusema kuwa sifa ya kwanza ya msanii kuwa katika usimamizi wa lebo ya WCB ni uwezo mzuri wa kuandika nyimbo sambamba na heshima na nidhamu ya kazi kama msanii.

 

Comments

comments

You may also like ...