Header

Kisses from Far Away: Familia ya Beckham ilivyofurahia maisha Serengeti

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya soka, Uingereza, David Beckham ametumia muda bora na familia yake katika mbuga ya wanyama ya Serengeti. Bechkam alikuja Tanzania wiki iliyopita akiwa na familia yake, wanae wanne na mke wake Victoria.

Imechukua muda kupost picha akiwa mbugani Serengeti hadi jana ambapo ameweka picha kadhaa.

Kwenye picha moja anaonekana akiwa amembeba na kumbusu mtoto wake wa mwisho wa kike, Harper Seven na kuandika, Kiss for Daddy ❤️.”

Ameweka pia video aliyomrekodi Simba aliyekuwa amelala kwenye majani na kuandika, WOW … So so beautiful.”

Naye mkewe Victoria, amepost picha ya mume na mwanae Brooklyn na kuandika, “Beautiful boys x kisses from far away ✨ love from the Beckham’s X #familytime 🙏🏻X VB.”

Mchezaji huyo wa zamani Manchester United na Real Madrid alikuja na wanae Brooklyn Beckham, Romeo James Beckham, Cruz David Beckham na Harper Seven Beckham.

Comments

comments

You may also like ...