Header

Ne-Yo adondosha wimbo mpya na kutangaza ujio wa Album

Mtayarishaji, muandishi na muimbaji Shaffer Chimere Smith a.k.a Ne-Yo baada ya kuachia ngoma yake mpya ‘Another Love Song’ ametangaza ujio wa Album yake mpya iliyopewa jina la ‘Good Man’

Kwa mujibu wa Ne-Yo kupitia kipindi cha Breakfast Club cha Power 105.1 FM ya mjini New York nchini Marekani, ameahidi kuwa katika aina yake ya ufanyaji kazi hajawahi kuwaangusha mashabiki hivyo watapata kitu kizuri ambacho tangu kuanza kwake katika kuachia utaratibu wake wa kazi na kuacha album ni sifa ya kazi nzuri pekee utawala hivyo ubora wa kazi zake hauna mabadiliko makubwa sana.

Akizungumzia ukimya wake Ne-Yo amesema kuwa tangu ukimya wake mpaka sasa amekuwa zaidi katika kujihusha na familia yake zaidi ambapo mwaka jana mwezi wa Machi pamoja na mkewe Crystal Renay walipata mtoto wao wa kiumeShaffer Chimere Smith Jr’.

“nimeoa, nimepata mtoto mwingine na nilitaka kuishi maisha ya kawaida kwa muda…ndoa, watoto na nimemaliza hilo na sasa ni muda…kutunza nyumba ni gharama, mtoto anahitaji pesa, kumjali mke wangu inahitaji pesa hivyo nahitaji kuachia muziki” Alisema Ne-Yo.

Ne-Yo ameongeza kuwa yuko katika umaliziaji wa album hiyo na kuitaja kuwa moja ya album zitakazo fanya vizuri kwasababu ya maadalizi mazuri na kuwa imesukwa katika lengo la kutoa burudani kama ilivyokawaida yake Pia album hiyo mbali na kuwa amaitangaza sasa lakini inategemewa mwezi September mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...