Header

Youngkiller atangaza idadi kamili kwa mwaka 2017

Rapa kutoka Matunzo Zero Unit na mkali wa ngoma ‘Sinaga Swagger Remix’ kutoka Tanzania Youngkiller Msodoki ametangaza idadi kamili ya kazi zitakazo toka mwaka huu kutoa kwake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Youngkiller ametangaza kuwa ni nyimbo tano pekee atakazoachia mwaka huu ikiwa amesha achia nyimbo mbili na kuwataka mashabiki wakae atayri kwa ujio wa ngoma nyingine ya tatu kati ya tano zilizoko katika utaratibu wa kutoka.

“MWAKA 2017 NitaachiA ngomA 5/= TU nA KatikA NgomA HIZO “TANO” MpakA SASA NimeachiA ngomA 2 TU /= 1) SINAGA SWAGGA “OG ”

2) SINAGA SWAGGA REMIX

#AmbazO kiukweli nafuraHI kwA map0kEZ yeNU makubwA katika ngomA zangU hizO naamin siku waangusHA Cos ngoma Nikali na HAKUNA HIP HOP yoyotE ambayO imetokA nikali kuzid ngomA HIZI” kwa MwakA huu 2017 “tutabishAnA mpakA kiamA 😊.. JE?! mpo tayarI kwA wimbO wangU wa 3…………………………….. ? kwA mwAkA huu 2017?! Youngkiller Alipost.

Hata hivyo kati ya ngoma ambazo zimesha tajwa kufanyika miongoni mwao ni kazi waliyofanya na rapa Khaligraph kutoka nchini Kenya igawa haijabainika kama ni ngoma inayofuata mbali na kuwa Youngkiller aliiambia Dizzim Online kuwa wako katika umaliziiaji wa Video.

Comments

comments

You may also like ...