Header

Diamond: Sallam ana mchango mkubwa mno kwenye muziki wa Tanzania

Diamond Platnumz ameamua kusema kitu ambacho hajawahi kumwambia meneja wake Sallam SK aka Mendez tangu aanze kufanya naye kazi. Hitmaker huyo wa Marry You anaamini kuwa Sallam ana mchango mkubwa si kwake tu na wasanii wa WCB, bali Tanzania kwa ujumla.

“Unajua kuna kitu ambacho Sallam sijawahi kumwambia hata siku moja katika kazi zetu na hata tukiwa tunapiga story kama kawaida lakini leo naona bora nimwambie kwamba ikitokea kesho au kesho kutwa akaanguka, simuombei mabaya lakini kila ikitokea hivyo mimi nitakuwa mtu kwanza kuhakikisha Watanzania na ulimwengu mzima kuwajuza kuwa Sallam alikuwa na mchango mkubwa, mkubwa sana katika kupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi,” ameiambia Dizzim Online.

Kwa upande mwingine, Diamond amesema tofauti na watu wengine wanavyodhani, Sallam si mtu mkali, bali ana msimamo kwenye kazi yake. “Watu wanatakiwa kutambua kuwa Sallam sio mkali isipokuwa hapendi kutumika hovyo pasipo maslahi au kuitumia WCB for free hapo lazima utamuona mkali,” ameongeza.

Comments

comments

You may also like ...