Header

Diana Edward yuko tayari kuingia kwenye uigizaji wa filamu

Ikiwa watu wengi sasa wamekuwa wakiisema vibaya tasnia ya filamu nchini na kupelekea hata wasanii wengine kusimama kufanya kazi kutokana na mambo tofauti tofauti yanayoendelea, hali ni tofauti kwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Edward. Mrembo huyo ameiambia Dizzim Online kuwa akipata nafasi ataingia kwenye uigizaji.

“Kuingia kwenye movie kwangu ni asilimia 75 nikipata tu nafasi, kwasababu pia kipindi cha nyuma nilikuwa kwenye kampuni ya waigizaji so nina uwezo mkubwa sana wa kuingia kwenye movie, ila hasa hasa zile za tofauti, yaani movie za tofauti zaidi, sio kama zile tulizozoea kuziona na ninaamini mi ni muigizaji mzuri sana ambaye naweza kuuvaa uhusika unaotakiwa,” amesema Diana.

Diana si miss pekee mwenye uwezo wa kuigiza. Wema Sepetu, Nargis Mohamed, Jokate Mwegelo, Irene Uwoya ni miongonu mwao.

Comments

comments

You may also like ...