Header

“Hatutaweka kambi nje ya nchi”: Azam Fc

Uongozi wa Klabu ya Azam Fc umeweka bayana kuwa kambi yao ya maandalizi ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao haitafanyika nje ya nchi badala yake wataendelea kujinoa katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na klabu hiyo kupitia kwa Msemaji wao Jaffari Iddi Maganga ambae amezungumza na waandishi wa Habari katika ofisi zao zilizopo Mzizima barabara ya Pugu jijini Dar es salaam. Iddy amesema kuwa timu hiyo haitaenda nje ya nchi kama walivyokua wanafanya miaka mingine.

“Hatutakua na kambi yoyote ya nje ya nchi, tutafanya kambi hapa, tutaiandaa timu hapa mpaka pale timu itapokuwa tayari kwa mechi za kirafiki na vile vile kuiandaa kwaajili ya Ligi kuu”. Alisema Jaffari Iddi.

Timu hiyo imetangaza pia majina ya wachezaji ambao wamemaliza miakataba yao klabuni hapo akiwemo Ame Alli Zungu pamoja na Mcha khamisi ambao wapo huru kujiunga na klabu yoyote.

Azam Fc itaingia kambini Julai 3 mwaka huu kujiandaa na michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi mapema mwezi wa nane.

Comments

comments

You may also like ...