Header

Queen Darleen atangaza mwezi rasmi wa ujio wake mwingine

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB Tanzania na hitamker wa ‘Kijuso’ aliyomshirikisha Rayvanny, Mwajuma Abdul a.k.a Queen Darleen amebainisha mwezi wa ukurasa mpya na muendelezo wa kuanza kuachia kazi kwa mwaka huu.

Akizungumza na Dizzim Online Queen amesema kuwa mpaka sasa katika uandaaji wa kazi mpya ambazo zitakuwa katika orodha ya kutoka zimekamilika tano ambapo tatu ziko tayari na video na mbili siku sio nyingi atasafiri  na uongozi kuelekea nchini Afrika Kusini kwa lengo la kukamilisha video za kazi hizo mbili na kubainisha kuwa mwezi wa nane ni mwezi wa kuanza kuachia kazi na biashara ya muziki itapamba moto zaidi kwa upande wake.

“mwezi wa Nane naanza balaa langu…Kolabo ziko haziwezi kukosa…nimefanya na msanii wa nje na hizi tatu zimeshootiwa hapa hapa Bongo na so far ningependa itoke kolabo kwasababu nawish…kwasababu ni hit song” Amesema Queen Darleen

Hata hivyo Queen ameacha menejimenti ifanye maamuzi ya ni kazi ipi itoke mbali na kuwa ameonekana zaidi kutamani kolabo itoke.

 

 

Comments

comments

You may also like ...