Header

Joh Maker athibitisha kutisha katika kila kolabo na Staa

Rapa na mkali wa michano na mwenye sifa ya kuandika ngumu baada ya kukubali kwenda na upepo wa biashara na kuja na ngoma ya maudhui ya malavi davi Joh Maker amezungumzia matokea na maoni ya kila anaposhirikishwa na msanii mkubwa katika kazi ambazo zimetangulia.

Maker ameiambia Dizzim Online kuwa kila hatua na jinsi anavyoachia kazi anawaza zaidi kuhakikisha hapotei katika muziki wa Tanzania na kote atakapofanikiwa kufika kwasababu ameona ni kwa kiasi kikubwa mashabiki na wadau wameanza kumuamini na kumpatia dhamana ya kuwakilisha kama msanii mwenye kipaji.

Hata hivyo Joh Maker ameonekana katika ushirikiano na wasanii wenye idadi kubwa ya mashabiki ambao ni pamoja na Youngkiller, Stamina, Quick Rocka, Godzilla na wengine ambapo katika kila ushirikiano ameonekana kuwa na uwezo mzuri.

Comments

comments

You may also like ...