Header

Picha: Ariana Grande awatembelea majeruhi wa shambulio la Manchester

Staa wa Marekani, Ariana Grande amesurprise mashabiki wake watoto waliojeruhiwa kwenye shambulio la Manchester Arena. Muimbaji huyo aliwakumbatia na kuzungumza na watoto hao wakiwa kwenye vitanda vyao vya hospitali wakati wakiendelea kupona kufuatia shambulio la wiki mbili zilizopita, kwenye show yake mjini Manchester. Watu 22 waliuawa.

Ariana amewasili Manchester Ijumaa hii kujiandaa na show ya Jumapili hii kwaajili ya wahanga na familia zao. Aliwatembelea watoto hao waliolazwa kwenye hospitali ya watoto ya Royal Manchester. Kwenye show ya leo iliyopewa jina,One Love Manchester, Grande ataungana na Justin Bieber, Katy Perry, Coldplay, Take That Miley Cyrus.

Tazama picha zaidi:

Comments

comments

You may also like ...