Header

Picha: Tamasha la hisani la Ariana Grande Manchester lafana ndani ya ulinzi mkali

Ariana Grande ametumbuiza Jumapili hii jijini Manchester, Uingereza kuwakumbuka wahanga wa shambulio la kigaidi kwenye show yake ya wiki mbili zilizopita katika mji huo.

Staa huyo alitoa heshima kwa mashabiki wake, akiwemo Olivia Campbell, 15, kwenye tamasha hilo la One Love lililofanyika kwenye uwanja wa cricket wa Old Trafford Cricket ambapo kauli mbili ilikuwa ‘Tunasimama Pamoja.’

Wengine waliotumbuiza ni Justin Bieber, Katy Perry, Coldplay, Pharrell Williams, the Black Eyed Peas, Usher, Robbie Williams, Little Mix na staa wa One Direction, Niall Horan. Wote walitumbuiza bure kukusanya walau paundi milioni 2 kwaajili ya We Love Manchester Emergency Fund.

Tamasha hilo limefanyika licha ya kuwepo shambulio jingine la kigaidi katika mji mkuu, London ambapo watu 7 waliuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya watu wawili kuwagonga watu kwenye daraja na kuanza kuwachoma visu.

Tazama picha zaidi:

Comments

comments

You may also like ...