Header

Ubingwa wa UEFA Real Madrid na historia yake

MILAN, ITALY - MAY 28: Sergio Ramos of Real Madrid of Real Madrid lifts the Champions League trophy after the UEFA Champions League Final match between Real Madrid and Club Atletico de Madrid at Stadio Giuseppe Meazza on May 28, 2016 in Milan, Italy. (Photo by Laurence Griffiths/Getty Images)

Klabu ya Real Madrid imetwaa ubingwa wa 12 wa mashindano ya UEFA Champion hapo jana baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya Juventus mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa wa timu ya Wales mjini Cardiff.

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo ambae alifunga magoli mawili, Casemiro pamoja na Marco Asensio huku Mario Mandzukic akifunga bao pekee kwa upande wa Juventus.

Baada ya kutwaa ubingwa huo klabu ya Real Madrid inakua klabu ya kwanza katika historia ya michuano hii ya UEFA kutetea taji hilo, walinyakua ubingwa msimu wa mwaka jana kwa kuifunga klabu ya Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati 5-3 nchini Italia. Zinedine Zidane ambaye ni kocha mkuu wa klabu hiyo anaingia katika historia ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji hilo mara mbili akiwa na miezi 16 tu katika klabu hiyo.

Mchezaji bora wa Dunia Cristiano Ronaldo ameweka pia rekodi katika mchezo wa jana ikiwemo kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo mara tano mfululizo kuanzia msimu wa 2013. Pia mchezaji huyo ni mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali nne za Mashindano haya ya UEFA mwaka 2008 akiwa na Manchester United, 2014,2016 pamoja na 2017 hapo jana. huku Nahodha wa klabu hiyo Sergio Ramos anakua ni nahodha wa kwanza kubeba taji la UEFA mara mbili mfululizo.

Real Madrid watakutana na Manchester United ambae ni bingwa wa Europa katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya UEFA msimu ujao.

Comments

comments

You may also like ...