Header

Hazard apata majeraha, hati hati kuikosa Arsenal

Chama cha soka nchini Ubeligiji RBFA kimethibitisha kuwa Kiungo wa Chelsea Eden Hazard ataukosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Czech Republic pamoja na ule wa kufuzu kucheza kombe la Dunia dhidi ya Estonia baada ya mchezaji huyo kupata majeraha ya “Enka” wakati akifanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ubeligiji hapo jana.

Hazard,26 ambaye ameisaidia klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligi kuu nchini Uingereza msimu huu 2016/2017 amefanyiwa vipimo nchini Ubelgiji ingawa bado taarifa ya muda atakaokaa nje ya uwanja nyota huyo haujatajwa.

Huenda Hazard akakosa baadhi ya mechi za mwanzo za msimu ujao ukiwemo mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Arsenal mwezi Agosti.

 

 

Comments

comments

You may also like ...