Header

Stamina akerwa na wabongo wanaoshangaa mwana hip hop kuimba mapenzi

Stamina ameamua kuwafungukia Watanzania wanaoshangazwa na kitendo cha msanii wa hip hop kama yeye kuimba mapenzi. Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake, Love Me aliyomshirikisha Maua Sama, ameiambia Dizzim Online kuwa watu wanatakiwa kufahamu msanii lazima abadilike ili kuwa na ladha tofauti tofauti.

“Hivi kwanini inakuwa hivi Tanzania? kwani sisi watu wa hip hop hatutakiwi kuimba mapenzi? Au mapenzi sio sehemu ya jamii?” amehoji. “Mashabiki wawe na fikra mpya, sisi ni waandishi na mwandishi anaandika chochote kile, huwezi kumpangia mwandishi cha kuandika.”

“Haimaanishi kwamba mtu wa hip hop asiimbe mapenzi kina 2 Pac huko wameimba mapenzi itakuwa sisi? Mapenzi ni sehemu ya jamii kuna kitu gani kikubwa kwenye jamii kama sio mapenzi? Sisi wenyewe tumezaliwa kwasababu ya mapenzi, mapenzi ndio kitu cha kwanza na vingine vinafuata lazima tuwe kwenye mapenzi,” amesisitiza.

Comments

comments

You may also like ...