Header

Stamina kuwashirikisha Nyashinski, Khaligraph na Avril

Stamina anataka kuufanya mwaka 2017 wa tofauti katika muziki wake. Amejipanga kuja na collabos tatu tofauti na wasanii wa Kenya.

Rapper huyo wa Morogoro, ameiambia Times FM kuwa hivi karibuni anasafiri kwenda Nairobi kufanya media tour akiongozana na Manecky na huko atarekodi ngoma na Khaligraph, Nyashinski na Avril.

Ameongeza pia kuwa atafanya video ya wimbo mmoja. Katika hatua nyingine rapper huyo amedai kuwa kila mwezi sasa atakuwa akiachia wimbo mpya.

Comments

comments

You may also like ...