Header

Dortmund yapata mrithi wa Tuchel

Klabu ya Borussia Dortmund kutoka Ujerumani imemtangaza Peter Bosz kuwa kocha mpya wa Klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili baada ya Thomas Tuchel kuachia ngazi klabuni hapo

Bosz,53 anaondoka katika klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi baada ya kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Europa ligi msimu huu.

Kocha huyo anakua Muholanzi wa pili kuifundisha timu hiyo baada ya Bert van Marwijk mwaka 2004. Dortmund wameshinda taji moja msimu uliopita ambalo ni kombe la ligi maarufu kama “DFP Pokal” huku wakimaliza nafasi ya tatu katika ligi msimu uliopita.

Comments

comments

You may also like ...