Header

Stars kutua kesho kutoka Misri

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kuondoka nchini Misri usiku wa kuamkia Jumatano kurejea jijini Dar es salaam baada ya kumaliza kambi ya wiki moja mjini Alexandria nchini humo.

Kikosi hicho cha wachezaji 23 kitawasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Africa, AFCON 2019 dhidi ya Lesotho utakaopigwa Juni 10 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

Timu hiyo chini ya Kocha mkuu Salum Mayanga imefanya mazoezi ya mwisho jioni ya leo na itaanza safari usiku huu ambapo inatarajiwa kutua uwanja wa ndege jijini Dar es salaam asubuhi ya siku ya jumatano.

 

Comments

comments

You may also like ...