Header

Timu ya Riadha Tanzania (RT) kujipiga msasa kambini

Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limethibisha maadalizi ya kukita kambi kwa timu ya taifa ya riadha kujiandaa na mashindano ya dunia.

Timu hiyo itatua kambini Julai 12 kujiandaa na mashindano ya dunia yatakayofanyika Kenya pamoja na yale ya England.

“Timu ya vijana itakwenda kwenye mashindano ya dunia Kenya na ile ya wakubwa itakuwa London, England, ” alisema Katibu mkuu wa shirikisho hilo la RT, Wilhelim Gidabuday.

“Timu ya wakubwa itakuwa Kenya kambini na timu ya vijana itabaki nchini ambapo watajifua katika viwanja vya Filbert Bayi,” ilifafanua taarifa ya RT.

Hata hivyo Makamu wa rais wa RT, Dk. Hamad Ndee alisema maandalizi ya kambi ya timu hizo yanakwenda vizuri ambapo wanariadha 12 wataiwakilisha nchi kwenye mashindano ya vijana huku kwenye timu ya wakubwa tayari wanariadha saba wamefuzu.

Comments

comments

You may also like ...