Header

Ujauzito wamtesa Linah ‘namiss vitu vingi’

Ikiwa wanawake wengi sana hushindwa kufanya majukumu yako kipindi cha ujauzito, msanii wa Bongo Flava Linah Sanga, ni mmoja wao. Kutokana na kuwa mama kijacho, muimbaji huyo ameshindwa kabisa kufanya shughuli zake hasa zinazohusiana na muziki.

Ameiambia Dizzim Online kuwa kwa kipindi anamiss vitu vingi ambavyo zamani alikuwa akivifanya.

“Kiukweli sasa hivi namiss vitu vingi sana, kwanza kazi yangu kipindi sipo mjamzito nilikuwa busy sana na kazi kutoa ngoma mpya, kufanya show, kutembea mikoani,” amesema. “Sasa hivi show nyingi zinanipita. Lakini sijutii kwasababu ni kitu ambacho mwenyewe nilikitaka, sikulazimishwa na mtu, so nafurahia hali hiyo na nawaomba mashabiki zangu waniombee nijifunguwe salama,” ameongeza.

Hivi karibuni Linah aliachia wimbo uitwao Upweke akiwa na Mr Kesho.

Comments

comments

You may also like ...