Header

Virgil van Dijk kuigharimu Liverpool

Klabu ya Southampton imepanga kupeleka mashitaka yake katika Bodi ya Ligi kuu Uingereza baada ya majogoo hao wa jiji kutumia njia zisizo sahihi katika kutaka kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk.

Liverpool haijapeleka ofa maalumu katika klabu ya Southampton kumtaka beki huyo ingawa kuna taarifa kuwa klabu hiyo tayari imeanza mazungumzo na mchezaji mwenyewe bila kupata ruhusa kutoka katika klabu yake ambayo ni kinyume na taratibu za usajili.

Beki huyo,25 amekuwa akihusishwa kuhamia Liverpool tangu msimu uliopita kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa ni Paundi milioni 50 licha ya kuwa na mkataba na Southampton wa miaka 6.

Muholanzi huyo hajaonekana uwanjani kipindi cha miezi mitano tangu alipopata majeraha katika mchezo waliopoteza kwa magoli 3 dhidi ya Leicester City Januari 22, amekosa michezo mingi ukiwemo wa fainali ya EFL Cup dhidi ya Manchester United Mwezi Februali mwaka huu.

Southampton pia imeripoti kuwa itagomea ofa yoyote maalumu itakayoletwa na Liverpool ikigundua ilianza mazungumzo na mchezaji huyo kabla.

 

 

Comments

comments

You may also like ...