Header

Mbeya City kutoa kipaumbele kwa wazawa kwanza

Klabu ya mpira wa miguu ya Mbeya City imehakikisha inatoa kipaumbele cha usajili kwa wachezaji wazawa wenye viwango katika mchakato huu wa za usajili wapya wa msimu mpya.

Kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo Godfrey Katepa imebainisha kuwa katika usajili na kuzingatia wazawa mpaka sasa usajili unaenelea vizuri.

“Siyo kwamba tupo kimya, mikakati inaendelea, lakini tumedhamiria kuimarisha kikosi chetu kwa kuangalia wachezaji wazawa,”alisema Katepa.

Hata hivyo katika kujihakikishia uimara wa kikosi mwezi ujao kocha mkuu wa timu hiyo Kinnah Phiri atarejea nchini kuaza maadalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu 2017/18.

Vile vile Klabu hiyo tayari imempoteza nahodha wake Kenny Ally ambaye amejiunga na Klabu ya Singida United.

 

 

 

 

 

 

 

Chanzo: Mwanaspoti

Comments

comments

You may also like ...