Header

Bahati arudia kinachozua maswali kila kolabo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya cha injili kutoka nchini Kenya Bahati ameendeleza mfumo wake wa kushirikiana na wasanii ambao hawako katika orodha ya wasanii wanaofanya muziki wa injili katika muziki wake.

Ikumbukwe mfumo huo ulileta maneno maneno ya kwanini kuna mchanganyiko wa aina hiyo jambo ambalo Bahati hajasita kabisa zaidi ameonekana kuongeza kolabo na wasanii wa nje ya injili.

Baada ya kolabo yake ya ‘Nikumbushe’ na msanii kutoka WCB Tanzania Rayvanny, hitmaker wa ngoma ya ‘Barua’ na ‘Mama’ ameachia kazi nyingine aliyomshirikisha mshindi wa tuzo ya BET kutoka Uganda Eddy Kenzo wimbo unaokwenda kwa jina ‘Barua kwa Mama’.

Katika orodha ya kolabo za namna hiyo Bahati mpaka sasa ameshirikiana na wasanii kama Rabbit Kaka Sungura,, Wyre, Rayvanny na Eddy Kenzo.

 

 

Comments

comments

You may also like ...