Header

Nuh Mziwanda hahitaji collabo za kimataifa kwa sasa

Nuh Mziwanda amesema hana mpango wa kufanya collabo na msanii wa nje ya Tanzania kwa sasa. Akiongeza na Dizzim Online, muimbaji huyo amesema anachokitaka ni kutengeneza muziki utakaopendwa kimataifa.

“Yaani mimi nasemaga kitu kimoja kila siku kuwa msanii kama msanii usipende kutegemea kufanya collabo nje ya nchi ndo ikufanye wewe utusue Kwasababu muziki ni ule ule. Tunasikiliza nyimbo za wazungu, hatuelewi maana wanavyoimba lakini tunapenda hits na melody basi. Kwahiyo usitegemee kufanya nyimbo na Chris Brown hata kama mbaya basi itafanya vizuri, haiwezi.”

Ameongeza, ” Lazima uangalie kwanza je hiki nachokifanya au kutengeneza ni cha international. Kwahiyo mimi ninachoamini ndani ya muziki wangu ninaoufanya naamini ni ladha na napata sms kutoka Nigeria wananisifia muziki wangu mzuri. So nashauri wasanii wenzangu waanze kwanza kufanya muziki wa ki international halafu ndo washirikishe hao wasanii wa nje.”

Nuh Mziwanda anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake Anameremeta.

Comments

comments

You may also like ...