Header

Shetta: Bongo tuna warembo wengi wa video lakini waoga

Msanii wa Bongo Flava, Shetta ametoa sababu ya yeye kwenda kufanya video nje ya Tanzania, kitu ambacho kwa sasa kimekuwa kawaida kwa wasanii wa Bongo. Amezitaja sababu hizi ikiwemo ya warembo wa Tanzania kuwa waoga.

Ameiambia Dizzim Online, “Mwanzo tulikuwa tunaenda kwasababu ya production, sasa hivi tunaona kwenye sekta ya production madirector wetu wanajitahidi sana. Kama mimi niliwahi kumchukua director nikaenda kufanya naye kazi kwa sababu wasanii wengi sana wa nchi tofauti wanadeal madirector wao.”

Aidha aliongeza na kusema, “Kingine kule kuna mandinga makali sana, so kama video yako inahitaji hivyo unajikuta huna jinsi unaenda tu kama bajeti ipo vizuri. Pia hata hawa ma video queen Bongo ni wale wale kila siku, inakuwa haileti maana sasa. Kiukweli Tanzania tuna mademu wakali lakini wengi wao ni waoga, sasa ukienda nje unakuta wapo wengi ni wewe tu kujichagulia.”

Comments

comments

You may also like ...