Header

Wizkid aupiga teke umaarufu

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid anayezendelea kufanya vizuri na kolabo ya wimbo wa Closer alimshirikisha Drake amebainisha kujitenga na fikra zenye jicho la umaarufu anapokuwa akifanya muziki wake.

Akipiga stori na MTV International Wizkid amesema kuwa siku zote haafanyi muziki kulewa umaarufu na support ya mashabiki na kuongeza kuwa kikubwa kwa support, mafanikio na umaarufu analionao anawashukuru sana kwa mchango wao mkubwa.

“Mimi sifanyi muziki kwa ajili ya umaarufu, sioni hilo kabisa, hivyo siachi hilo likatawala kichwa changu, mimi nikozaidi katika muziki” Alisema Wizkid.

Hata hivyo ameshabainisha kuwa katika album yake ambayo imekamilika kwa kiasi kikubwa ameshirikiana na wakali kama Drake, Chris Brown, Trey Songz, Diplo, Ty Dolla Sign wengine wengi.

Comments

comments

You may also like ...