Header

CAF yataja waamuzi mchezo wa Stars na Lesotho

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud, ambaye ni mwamuzi wa kati huku wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia.

Waamuzi hao pamoja na kamishna wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho Ijumaa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya wakati wapinzani wa Taifa Stars wanaingia jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

Mchezo kati ya Taifa Stars na Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam uliko Chamazi, Dar es Salaam. Mchezo huo dhidi ya Lesotho utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Mbali ya Lesotho na Tanzania, Mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, watakuwa katika michezo yao ya kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

Comments

comments

You may also like ...