Header

Shetta aanza kutimiza azma yake katika mwezi mtukufu wa Ramadhan

Ukizungumzia wasanii walioutumia mwezi huu mtukufu wa mfungo wa Ramadhani katika kujitolea kijamii lazima utamtaja msanii Nurdin Bilal anayefahamika zaidi kama Shetta kwakuwa siku chache kabla ya mwezi huu alitangaza na kutoa njia sahihi kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa kila kituo chenye watoto wenye uhitaji wa mahitaji muhimu watume maombi yao.

 

Mbele ya kamera za Dizzim Online Shetta leo ameitumia siku yake kwa kutembelea vituo vitatu tofauti vya watoto wenye uhitaji vilivyoko jijini Dar es salaam ambavyo ni ‘Meta meta Orphanage kilichoko Bunju, New Life Orphanage Centre kilichoko Boko na Maunga Centre kilichiko wilaya ya Kinondoni ambapo amechangia mahitaji ya matumizi ya kila siku pamoja na vyakula.

Hata hivyo uchangiaji huo wa Shetta mbali na kuwa amefanya hivyo kwa nguvu na mchango wa uongozi wa menegimenti yake iliyoongozwa na ‘Michael Mlingwa‘ Mx Cater ameshirikiana na Mo Dewji Foundation ambapo kwa mujibu wa Shetta amebainisha kuwa kampeni ya uchangiaji huo imeanza rasmi leo.

 

Kwvideo na picha zaidi endelea kufatilia Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...