Header

Vanessa Mdee yuko tayari kuingia kwenye Bongo Movie

Baada ya kufanya vizuri kwenye tamthilia ya MTV Shuga, Vanessa Mdee amefikiria kujiimarisha zaidi kwenye uigizaji. Tumemfuta kutaka kufahamu kama anaweza kuingia kabisa kwenye filamu hususan za Tanzania.

“Kiukweli napenda kazi za nyumbani na nikipata nafasi nina uwezo mkubwa sana wa kufanya filamu ya Kitanzania au tamthiliya ya Kitanzania ambayo ina ubora mzuri na maslahi,” ameiambia Dizzim Online. “Lazima nifanye kwasababu nataka nijikite kwenye filamu taratibu nikijifunza vingine na ili niweze kuwa bora zaidi. Lakini mpaka sasa sijapata hiyo nafasi na nikiipata lazima nitafanya,” ameongeza.

Vanessa amesifiwa sana kwa uhusika wake kama Storm kwenye MTV Shuga.

Comments

comments

You may also like ...