Header

Bahati ataja BET Awards na MTV kuwa ni ndoto katika injili yake

Msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya anayefanya vyema na wimbo wake ‘Barua kwa Mama’ aliomshirikisha msanii kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo, Bahati ametaja kuwa tuzo ya BET kama moja ya ndoto yake kama msanii kama atazidi kupata support kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau.

Akizungumza kupitia Radio Maisha ya nchini Kenya, Bahati amesema kuwa anatamani kuwa msanii wenye uwezo wa kuwa sauti kila mtoto barani Afrika hata kuongeza kuwa ni tamaa yake kubwa kuwa msanii wa kwanza wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya kushinda tuzo ya BET au MTV.

“Dream yangu kubwa ambayo ningependa watu waelewe…mimi ningependa niwe msanii wa kwanza wa Gospel kuwin…kuleta BET Awards nyumbani ama MTV Awards nyumbani na ninaona pengine na make moves” Alisema Bahati.

Hata hivyo Bahati ameongeza kuwa baada ya kufanya wimbo na msanii Rayvanny wa ‘Nikumbushe’ kisha kuachia wimbo aliomshirikisha Eddy Kenzo kutoka Uganda amethibitisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili ataachia wimbo mwingine na msanii kutoka Tanzania.

Comments

comments

You may also like ...