Header

Dj Khaled amkabidhi ofisi mwanae wa Miezi 7 ‘Asahd’

Rapa, mtayarishaji, Dj na mmiliki wa lebo ya muziki ya ‘We the Best Music Group’ kutoka Marekani anayetegemea kuachia album yake ya 10 inayokwenda kwa jina la ‘Grateful’ tarehe 23 ya mwezi huu ameonesha wazi ofisi ya mwanae Asahd Tuck Khaled mabali a kuwa ana umri ndogo.

Kupiti mitandao ya kijamii ya Dj Khaled kila leo hasa ule wa snapchat hakosi kuwa na jipya ambapo juzi kati alitoa taarifa ya picha ya cover ya ujio wa album ya Grateful ambao ilipambwa kwa picha ya mwanae Asahd na mara hii amepost picha tofauti tofauti za maeneo tofauti ya ofisi huku  zikiwa ni picha ambazo zilieleza kuwa ni ofisi ya mwanae Asahd ambaye kwasasa ni mwenye umri wa miezi saba 7.

Hata hivyo Dj Khaled katika kukamilisha ujio wa album alibainisha kuwa Asahd amehusika kama mtayarishaji mtendaji (Executive Producer) wa album ya Grateful inayotegemewa kuwa na ngoma 23 kali.

Comments

comments

You may also like ...