Header

Kane kuvaa kitambaa cha Rooney Uingereza

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane ameteuliwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate kuwa nahodha wa mchezo wa leo wa kimataifa dhidi ya Scotland.

Kane,23 ataiongoza Uingereza katika mchezo wa kufuzu kucheza fainali ya kombe la Dunia mwaka 2018, mchezo utakaopigwa katika dimba la Hampden ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Scotland.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kane kuiongoza timu hiyo kama Nahodha baada ya Wayne Rooney ambae ni nahodha wa kudumu wa kikosi hicho kuachwa na kocha mkuu. Awali nahodha aliyeshikilia kitambaa hicho alikua ni Jordan Henderson wa Liverpool ambaye ni majeruhi pia.

Mchezo huu ni wa kwanza kwa Harry Kane kwa timu ya taifa tangu tarehe 4 Septemba 2016 kutokana na majeruhi, nyota huyo alitangazwa kuwa mfungaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu 2016/2017 baada ya kufunga magoli 29 huku akiwa na jumla ya magoli 35 katika michezo 39 aliyocheza.

Comments

comments

You may also like ...