Header

Mrembo wa Rayvanny ashindwa kusimama robo tatu ya video ya ‘Mbeleko’

Msanii wa muziki kutoka lebo ya muziki Tanzaniay WCB ‘Rayvanny’, baada ya kupeta uzuri kabisa na ngoma yake ya ‘Zezeta’ amepakua video ya wimbo mwingine unaokwenda kwa jina la ‘Mbeleko’ video ambayo imeoneana kuwa na ubora na ubunifu zaidi chini ya uongozaji wa Director Joowzey.

Kupitia video ya wimbo huo imeonekana kuwa Rayvanny mwenye kumjali zaidi mrembo ambaye ni mpenzi wake(Katika Video) ambaye alipata ajali alipokuwa kivuka barabara kuelekea upande wa pili wa barabara kumpokea Rayvanny mizigo ambayo alitoka kuinunua tukio ambalo lilimlazimu director kutomuonesha tena mrembo huyo akiwa amesimama kwa mujibu wa ubunifu katikanafasi aliyotumika.

Hata hivyo video hii inaweza kutajwa kuwa moja ya video zenye ubunifu wa haina yake kutoka kwa muongozaji Joowzey kutoka Tanzania hata kuonekana kuwa na muonekano mzuri wa picha kaisi cha kuchangia pakubwa katika kuwashawishi wasanii kutoka Afrika Mashariki kupunguza kaam sio kucha kabisa safari za Bondeni kwa ajili ya kushoot video kali.

Itazame Video hapa chini.

Comments

comments

You may also like ...