Header

Upweke nje ya Yamoto Band wamtesa Enock Bella

Msanii wa Yamoto Band, Enock Bella ameelezea ugumu anaoupata baada ya kuanza kufanya kazi kama solo artist. Akipiga story na Dizzim Online msanii huyo wenye ladha ya kipekee amesema alizoea kufanya kazi kama kundi.

“Kwanza ugumu ulikuja kwenye mazoea,” amesema. “Mazoea ni kitu kimoja kibaya sana jinsi tulivyokaa pamoja kwa muda mrefu kabla ya Yamoto Band mpaka ikawa Yamoto Band. So kuna vitu vingi kwa sasa nakosa kama utani ule, sasa hivi siupati tena. Pia ilikuwa vigumu sana kupata management mara moja kwasababu walihisi bado tupo kwa Mkubwa na wanajua kuwa Mkubwa sio mtu wa kawaida yaani mtu aje kuongea na msanii wake kazi bila kupitia kwakwe inakuwa ngumu lakini kwa sasa nimepata wasimamizi wananisimamia,” ameongeza.

Enock Bella ameachia ngoma yake mwenyewe iitwayo Mkuyu ambayo hata hivyo amesema haikutoka rasmi.

Comments

comments

You may also like ...