Header

Zlatan Ibrahimovic kuendelea kusalia Man U

Licha ya Manchester United kutangaza kuachana na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka atakapopona majeraha yake.

Uongozi wa United utaendelea kuhudumia na kushughulikia gaharama za matibabu yote ya mchezaji huyo mpaka atakapoamua kuondoka klabuni hapo au akipata timu nyingine.

Ibrahimovic, 35 aliumia katika mchezo wa kombe la Europa dhidi ya Anderlecht mwezi April ambayo yamemfanya kukosa michezo muhimu katika klabu ya Manchester United ukiwemo ule wa Fainali ya Europa dhidi ya Ajax uliopigwa Sweeden ambako Zlatan alizaliwa.

United imetangaza kutomuongezea mkataba Zlatan baada ya ule wa mwanzo kumalizika. mchezaji huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja mpaka mapema mwakani, 2018. Klabu ya Manchester United inatajwa kuwa katika mazungumzo na mchezaji Alvaro Morata wa Real Madrid pamoja na Andrea Belloti wa Torino ili kuziba pengo la Ibrahimovic.

Comments

comments

You may also like ...