Header

Nasty C aachia hii nyingine kwa upendo wa marehemu mama yake mzazi

Mkali na rapa mchanga, wenye umaarufu na wenye umri mdogo kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika zaidi kama ‘Nasty C’ ambaye amefanya vyema zaidi na ngoma ya ‘Juice Back Remix’ ameachia video mpya ya kazi ambayo maudhui yake yanamlenga marehemu mama yake mzazi.

Nasty mwwenye umri wa miaka 20 amewahi kusimulia kuwa hakubahatika kumuona mama yake mzazi kwa kuwa mzazi wake huyo alifariki kipindi ambacho Nasty C alikuwa ni mwenye umri wa miezi 11, miaka 20 iliyopita umri ambao hakuweza kumuona na kumtambua wala kuzungumza naye zaidi ya kumuona tu kwenye picha akiwa katika umri wa utoto wa ufahamu na utu uzima.

Hata hivyo kazi hii ni ngoma iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana kama audio ambapo video imeongozwa na aliyeshiriki ia kuongoza ngoma ya rapa huyo ya ‘Bad hair’ director ‘Emilie Badenhorst’ & ‘Nani Chehore’ kisha kueditiwa kwa ushirkianao wa Nani na Nasty C mwenye ngoma ambayo iko katika orodha ya ngoma 19 zinazokamilisha Album yake ya ‘Bad Hair Extensions’.

Comments

comments

You may also like ...