Header

Video: Mrembo aokelewa na polisi Dar baada ya kutaka kuvuliwa nguo hadharani kwa kuvaa kimini

Mrembo mmoja amenusurika kuvuliwa nguo hadharani jijini Dar es Salaam baada ya kuvaa kimini kilichokuwa kimeacha sehemu kubwa ya mapaja yake meupe nje. Video iliyosambaa mtandaoni, inamuonesha msichana huyo aliyevaa mini skirt nyeupe yenye mistari mieusi na mkoti mwekundu akiwa amekimbilia kwenye mgahawa wa nje kuepuka vijana wenye hasira waliokuwa wakimzomea na kutaka kumvulisha nguo zake.

Mrembo huyo alinusurika kudhalilika baada ya polisi kufika eneo la tukio linalodaiwa kuwa ni Kariakoo na kumuokoa. Video inamuonesha msichana huyo aliyejazia kweli kweli akitembea kwa tabu kujaribu kuivuta sketi yake fupi kuficha maungo yake. Itazame video hiyo hapo chini.

Comments

comments

You may also like ...