Header

Bahati baada ya Rayvanny na Eddy Kenzo amuongeza Stone Bwoy

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya Kelvin Bahati a.k.a Bahati baada ya kolabo yake na msanii kutoka Uganda ‘Eddy kenzo’, amethibitisha kolabo nyingine na staa wa Afro-pop, Dancehall na reggae kutoka nchini Ghana na ‘Stone Bwoy’.

Akipiga stori kupitia Radio Maisha Bahati amesema kuwa hakika ndoto zake za kuwa mwenye sauti kwa watoto barani Afrika ziko njia kutimia kwakuwa baada ya kolabo yake na Rayvanny na Eddy Kenzo anategemea kuachia kolabo nyingine aliyomshirikisha Stone Bwoy.

“na bado…na-drop song na Stone Bwoy from Ghana…nafeel ni Godly na ni Connected” Alisema Bahati.

CEO wa ‘Burniton Music Group ‘Stone’ na mshindi wa tuzo ya BET kutoka Afrika Mashariki Eddy Kenzo walikukutana na Bahati nchini Kenya katika msimu wa nne wa Coke Studio mwaka jana msimu ambao kuna uwezekanao kuwa uliwakutanisha na ni kipindi ambacho wakautumia vizuri muda huo katika kuhakikisha wanapanua wigo wa muziki wao na kuwafikia mashabiki wanaowalenga kwa njia ya kushirikiana.

Comments

comments

You may also like ...